Nokia X71 user guide

Skip to main content
All Devices

Nokia X71

Bluetooth®

Unaweza kuuunganisha pasi waya kwenye vifaa vingine vinavyotangamana, kama vile simu, kompyuta, vifaa vya sauti, na vifaa vya gari. Unaweza pia kutuma picha zako kwa simu zinazotangamana au kwenye kompyuta yako.

Unganisha kwenye kifaa cha ziada cha Bluetooth

Unaweza kuunganisha simu yako na vifaa vingi muhimu vya Bluetooth. Kwa mfano, na vifaa vya sauti vya pasi waya (kinauzwa kando), unaweza kuongea na simu bila kutumia mikono - unaweza kuendelea unachofanya, kama kufanya kazi kwenye kompyuta, wakati wa simu. Kuunganisha simu kwenye kifaa cha Bluetooth huitwa kuoanisha.

  1. Gusa Mipangilio > Vifaa vilivyounganishwa > Mapendeleo ya muunganisho > Bluetooth.
  2. Badilisha Bluetooth kwa Washa.
  3. Hakikisha kifaa kingine kimewashwa. Huenda ukahitajika kuanzisha mchakato wa kuoanisha kutoka kwenye kifaa kingine. Kwa maelezo zaidi, angalia mwongozo wa kifaa hicho kingine.
  4. Ili kuoanisha simu yako na kifaa, gusa kifaa kwenye orodha ya vifaa vilivyogunduliwa vya Bluetooth.
  5. Huenda ukahitaji kucharaza alamasiri za ruhusa. Kwa maelezo zaidi, angalia mwongozo wa kifaa hicho kingine.

Kwa kuwa vifaa vyenye teknolojia pasi waya ya Bluetooth huwasiliana kwa kutumia mawimbi ya redio, havihitaji kuwa vinaangaliana. Hata hivyo, lazima vifaa vyako vya Bluetooth viwe mita 10 (futi 33) na kifaa kile kingine, ijapokuwa muunganisho unaweza kuathiriwa na vizuizi kama vile kuta au kutoka vifaa vingine vya elektroniki.

vifaa vilivyolinganishwa vinaweza bado kuunganishwa kwenye simu yako wakati Bluetooth imewashwa. Vifaa vingine vinaweza kugundua simu yako tu ikiwa mwonekano wa mipangilio ya Bluetooth imefunguliwa.

Usilinganishe au kukubali maombi ya muunganisho kutoka kwa kifaa kisichojulikana. Hii husaidia kulinda simu yako dhidi ya maudhui mabaya.

Ondoa uoanishaji

Ikiwa huna kifaa ulichooanisha na simu yako, unaweza kuondoa uoanishaji huo.

  1. Gusa Mipangilio > Vifaa vilivyounganishwa > VIFAA VILIVYOUNGANISHWA AWALI.
  2. Gusa settings kando ya jina la kifaa.
  3. Gusa SAHAU.

Unganisha kwenye simu ya rafiki yako kwa kutumia Bluetooth

Unaweza kutumia Bluetooth pasi waya kuunganisha kwenye simu ya rafiki yako, ili kushiriki picha, na zaidi.

  1. Gusa Mipangilio > Vifaa vilivyounganishwa > Mapendeleo ya muunganisho > Bluetooth.
  2. Hakikisha Bluetooth imewashwa katika simu zote.
  3. Hakikisha simu zote zinaonekana kwenye zingine. Unahitaji kuwa katika mwonekano wa mipangilio ya Bluetooth kwa simu yako kuonekana kwenye simu zingine.
  4. Unaweza kuona simu za Bluetooth zilizo karibu. Gusa simu unayotaka kuunganisha.
  5. Ikiwa simu inahitaji msimbosiri, uaandike au kubali msimbosiri, na uguse Oanisha.

Msimbosiri hutumika tu wakati unaunganisha kifaa kwa mara ya kwanza.

Tuma maudhui yako kwa kutumia Bluetooth

Wakati unataka kushiriki maudhui yako au kutuma picha ulizopiga kwa rafiki, tumia Bluetooth kuzituma kwenye vifaa vinavyotangamana,

Unaweza kutumia zaidi ya muunganisho mmoja wa Bluetooth kwa wakati mmoja. Kwa mfano, wakati unatumia vifaa vya sauti vya Bluetooth, unaweza bado kutuma vitu vingine kwenye kifaa kingine.

  1. Gusa Mipangilio > Vifaa vilivyounganishwa > Mapendeleo ya muunganisho > Bluetooth.
  2. Badilisha Bluetooth kwa Washa.
  3. Nenda kwenye maudhui unayotaka kutuma, na uguse share > Bluetooth.
  4. Gusa kifaa unachotaka kuunganisha. Unaweza kuona vifaa vya Bluetooth vilivyo karibu.
  5. Kama kifaa kinahitaji msimbosiri, charaza msimbosiri huo. Msimbosiri, ambao unaweza kuubuni, lazima uwekwe kwenye vifa vyote. Msimbosiri katika vifaa vingine huwa vimewekwa. Kwa maelezo zaidi, angalia mwongozo wa kifaa hicho kingine.

Eneo la faili zilizopokewa hutegemea kifaa kile kingine. Kwa maelezo zaidi, angalia mwongozo wa kifaa hicho kingine.

Did you find this helpful?
  • Sasisha simu yako
  • Vitufe na sehemu
  • Ingiza au ondoa SIM na kadi ya kumbukumbu
  • Chaji simu yako
  • Washa na usanidi simu yako
  • Dual SIM settings
  • Kuweka ID ya alama ya kidole
  • Funga au fungua simu yako
  • Tumia skrini ya mguso
Intaneti na miunganisho
  • Amilisha Wi-Fi
  • Tumia muunganisho wa data ya simu
  • Vinjari wavuti
  • Funga muunganisho
  • Bluetooth®
  • VPN

Useful Links

PDFSoftware Updates

Countries and Languages

Contact the support team

Chat with us

Before starting chat with our customer support, please leave your contact details. Contact our chat support for online purchases support, product information, warranty support.

Start chat

Chat with us

Before starting chat with our customer support, please leave your contact details. Contact our chat support for online purchases support, product information, warranty support.

Fields marked with an asterisk are mandatory.

Your personal data will be processed according to HMD Global’s Privacy Policy and the HMD Support Supplement.

Email us

Tell us about your problem and we'll get back to you via email.

Contact us

Care centers

Prefer to bring your device in for our experts to have a look at? Find the location of your nearest Nokia & HMD phones, tablets and accessories care center.

Find a care center near you