Nokia X71 user guide

Skip to main content
All Devices

Nokia X71

Habari ya utoaji cheti (SAR)

Kifaa hiki cha mkononi kinatimiza maelekezo yanayohusu ujiwekaji wazi kwa mawimbi ya redio.

Kifaa chako cha mkononi ni transmita na kipokezi cha redio. Kimeundwa kisizidishe viwango vya ufichuzi vya mawimbi ya redio (maeneo ya mawimbi ya redio ya sumaku ya umeme), vinavyopendekezwa na miongozo ya kimataifa kutoka kwa shirika huru la kisayansi ICNIRP. Maelekezo haya yanajumuisha viwango vya usalama vilivyoundwa kuhakikisha usalama wa watu wote, Haijalishi umri na afya. Maelekezo ya ufichuzi yanategemea Kiwango Maalum cha Ufyonzaji (SAR), ambacho ni onyesho la nguvu ya kiwango cha masafa ya redio (RF) ambayo inawekwa kichwani au mwilini wakati kifaa kinatumika. Kiwango cha SAR cha ICNIRP cha vifaa vya simu ni 2.0 W/kg kwa wastani wa gramu kumi za tishu.

Vipimo vya SAR vinatekelezwa kwa kifaa katika mikao ya kawaida ya uendeshaji, wakati kifaa kinapitisha katika kiwango chake cha juu zaidi kilichoidhinishwa cha nishati, katika bendi zote zilizopimwa za masafa.

Kifaa hiki kinatimiza matakwa ya maelekezo ya ujiwekaji wazi kichwani au wakati kimewekwa angalau inchi 5/8 (sentimita 1.5) kutoka kwenye mwili. Wakati kikasha cha kubebea, kishikiza kwenye mkanda au aina nyingi ya kishikizi kikitumika kwa matumizi ya kuvaliwa mwilini, kinatakiwa kisiwe na chuma na kinatakiwa kuweka angalia umbali uliotajwa hapo juu kutoka kwenye mwili.

Kutuma data au ujumbe, muunganisho salama wa mtandao unahitajika. Utumaji unaweza kucheleweshwa hadi muunganisho huo upatikane. Fuata maagizo ya umbali wa kutenganisha hadi utumaji ukamilike.

Wakati wa matumizi ya kawaida, thamani za SAR kwa kawaida huwa chini ya thamani zilizotajwa hapa juu. Hii ni kwa sababu, kwa malengo ya ubora wa mfumo na kupunguza mwingiliano kwenye mtandao, nguvu ya kufanya kazi ya kifaa chako cha mkononi hupunguzwa kiotomati wakati nguvu kamili haihitajiki kwa simu. Nguvu towe inavyoendelea kuwa chini, ndivyo thamani ya SAR inavyokuwa chini.

Huenda modeli za vifaa zikawa na matoleo tofauti na zaidi ya thamani moja. Mabadiliko ya vijenzi na muundo yanaweza kufanyika baada ya muda na baadhi ya mabadiliko yanaweza kuathiri thamani za SAR.

Kwa maelezo zaidi, nenda kwenye www.sar-tick.com. Kumbuka kwamba vifaa vya mkononi huenda vikapitisha hata kama hupigi simu.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kwamba maelezo ya sasa ya kisayansi hayaashirii hitaji la tahadhari zozote maalum wakati wa kutumia vifaa vya mkononi. Ikiwa unavutiwa na kupunguza ufichuzi wako, wanapendekeza upunguze matumizi yako au utumie kifaa kisichotumia mikono ili kuweka kifaa mbali na kichwa na mwili wako. Kwa maelezo zaidi na ufafanuzi na majadiliano kuhusu ufichuzi wa RF, nenda kwenye tovuti ya WHO kwenye www.who.int/health-topics/electromagnetic-fields#tab=tab_1.

Tafadhali rejelea www.hmd.com/sar kwa thamani ya juu ya SAR ya kifaa.

Did you find this helpful?
  • Sasisha simu yako
  • Vitufe na sehemu
  • Ingiza au ondoa SIM na kadi ya kumbukumbu
  • Chaji simu yako
  • Washa na usanidi simu yako
  • Dual SIM settings
  • Kuweka ID ya alama ya kidole
  • Funga au fungua simu yako
  • Tumia skrini ya mguso
Maelezo ya bidhaa na usalama
  • Kwa usalama wako
  • Huduma za mtandao na gharama
  • Simu za dharura
  • Kuhudumia kifaa chako
  • Uchakataji upya
  • Alama ya pipa iliyo na mkato
  • Maelezo ya betri na chaja
  • Watoto wadogo
  • Vifaa vya matibabu
  • Vifaa vya matibabu vinavyopachikwa
  • Vifaa vya kusaidia kusikia
  • Linda mtoto wako dhidi ya vitu vyenye madhara
  • Magari
  • Mazingira yanayoweza kulipuka
  • Habari ya utoaji cheti (SAR)
  • Kuhusu Usimamizi wa haki za Dijitali
  • Hakimiliki na ilani

Useful Links

PDFSoftware Updates

Countries and Languages

Contact the support team

Chat with us

Before starting chat with our customer support, please leave your contact details. Contact our chat support for online purchases support, product information, warranty support.

Start chat

Chat with us

Before starting chat with our customer support, please leave your contact details. Contact our chat support for online purchases support, product information, warranty support.

Fields marked with an asterisk are mandatory.

Your personal data will be processed according to HMD Global’s Privacy Policy and the HMD Support Supplement.

Email us

Tell us about your problem and we'll get back to you via email.

Contact us

Care centers

Prefer to bring your device in for our experts to have a look at? Find the location of your nearest Nokia & HMD phones, tablets and accessories care center.

Find a care center near you