Mwongozo wa watumiaji wa Nokia 3310 3G

Skip to main content
All Devices

Nokia 3310 3G

Sanidi na uwashe simu yako

Jifunze jinsi ya kuingiza SIM kadi, kadi ya kumbukumbu, na betri, na jinsi ya kuwasha simu yako.

SIM Ndogo

SIM Ndogo
Muhimu: Kifaa hiki kimeundwa ili kutumiwa na SIM kadi ndogo pekee tu (angalia mfano). Matumizi ya kadi zisizotangamana za SIM zinaweza kuharibu kadi au kifaa, na zinaweza kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi. Tafadhali wasiliana na opereta wa simu yako kwa matumizi ya SIM kadi ambayo ina mkato wa nano-UICC.

Kadi za kumbukumbu za MicroSD

Kadi za kumbukumbu za MicroSD

Tumia tu kadi za kumbukumbu zinazotangamana zilizoidhinishwa kutumiwa na kifaa hiki. Kadi zisizotangamana zinaweza kuharibu kadi na kifaa na kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.

Kumbuka: Zima kifaa na usiiunganishe na chaja au kifaa kingine chochote kabla ya kubandua vifuniko vyovyote. Epuka kugusa visehemu vya elektroniki wakati wa kubadilisha vifuniko vyovyote. Daima hifadhi na kutumia kifaa kikiwa na vifuniko vyake vimewekwa.

Sanidi na uwashe simu yako (SIM moja)

Sanidi na uwashe simu yako (SIM moja)
  1. Weka kucha yako ya kidole katika nafasi ndogo chini ya simu, inua na uondoe kifuniko.
  2. Ikiwa betri iko ndani ya simu, itoe.
  3. Telezesha SIM kwenye kipenyo cha SIM eneo la mguso likiangalia chini.
  4. Ikiwa una kadi ya kumbukumbu, telezesha kadi ya kumbukumbu kwenye nafasi ya kadi ya kumbukumbu.
  5. Lainisha maeneo ya mguso ya betri, na uweke betri ndani.
  6. Rejesha kifuniko cha nyuma.

Sanidi na uwashe simu yako (SIM mbili)

Sanidi na uwashe simu yako (SIM mbili)
  1. Weka kucha yako ya kidole katika nafasi ndogo chini ya simu, inua na uondoe kifuniko.
  2. Ikiwa betri iko ndani ya simu, itoe.
  3. Telezesha SIM ya kwanza kwenye kipenyo cha SIM 1 eneo la mguso likiangalia chini. Telezesha SIM ya pili kwenye kipenye cha 2 cha SIM. SIM kadi zote zinapatikana kwa wakati mmoja wakati kifaa hakitumiki, lakini ijapokuwa SIM kadi moja inatumika, kwa mfano, kwa kupiga simu, ile nyingine haipatikani.
  4. Ikiwa una kadi ya kumbukumbu, telezesha kadi ya kumbukumbu kwenye nafasi ya kadi ya kumbukumbu.
  5. Lainisha maeneo ya mguso ya betri, na uweke betri ndani.
  6. Rejesha kifuniko cha nyuma.

Washa simu yako

Bonyeza na ushikilie kitufe cha .

Ondoa SIM kadi

Fungua kifuniko cha nyuma, ondoa betri, na uondoe SIM.

Ondoa kadi ya kumbukumbu

Fungua kifuniko cha nyuma, ondoa betri, na utoe kadi ya kumbukumbu.

Misimbo ya ufikiaji

Simu yako na SIM kadi hutumia misimbo tofauti ya usalama.

  • Misimbo ya PIN au PIN2: Misimbo hii hulinda SIM kadi yako dhidi ya matumizi yasiyoidhinishwa. Ukisahau misimbo au iwe haijatolewa pamoja na kadi yako, wasiliana na mtoa huduma wa mtandao wako. Ukicharaza msimbo vibaya mara 3 zikifuatana, unahitaji kufungua msimbo kwa kutumia msimbo wa PUK au PUK2.
  • Misimbo ya PUK au PUK2: Misimbo hii inahitajika ili kufungua msimbo wa PIN au PIN2. Ikiwa misimbo haijatolewa na SIM kadi yako, wasiliana na mtoa huduma wako wa mtandao.
  • Msimbo wa usalama: Msimbo wa usalama hukusaidia kulinda simu yako dhidi ya matumizi yasiyoidhinishwa. Unaweza kuweka simu yako kukuuliza msimbo wa usalama ambao unafasili. Weka msimbo kuwa siri na mahali salama, kando na simu yako. Ukisahau msimbo na simu yako imefungwa, simu yako itahitaji huduma. Huenda gharama ya ziada ikatumika, na data yote ya kibinafsi kwenye simu huenda ikafutwa. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na care point iliyo karibu ya simu yako, au muuzaji wa simu yako.
  • Msimbo wa IMEI: Msimbo wa IMEI hutumiwa kutambua simu katika mtandao. Huenda pia ukahitaji kupeana nambari kwa huduma zako za care point au muuzaji wa simu. Ili kuona nambari yako ya IMEI, piga *#06#. Msimbo wa IMEI wa simu yako umechapishwa pia kwenye lebo ya simu yako, ambayo iko chini ya betri. IMEI inaonekana pia kwenye sanduku halisi la mauzo.
Did you find this helpful?
Anza kutumia
  • vitufe na sehemu
  • Sanidi na uwashe simu yako
  • Chaji simu yako
  • Funga au fungua vitufe

Useful Links

PDFSoftware Updates

Countries and Languages

As we offer product user guides in many languages across different regions, you may be redirected to a Nokia phones web page outside of your selected location.

Countries and Languages

Choose Language

Contact the support team

Chat with us

Before starting chat with our customer support, please leave your contact details. Contact our chat support for online purchases support, product information, warranty support.

Start chat

Chat with us

Before starting chat with our customer support, please leave your contact details. Contact our chat support for online purchases support, product information, warranty support.

Fields marked with an asterisk are mandatory.

Your personal data will be processed according to HMD Global’s Privacy Policy and the HMD Support Supplement.

Email us

Tell us about your problem and we'll get back to you via email.

Contact us

Care centers

Prefer to bring your device in for our experts to have a look at? Find the location of your nearest Nokia & HMD phones, tablets and accessories care center.

Find a care center near you