Muhimu: Epuka kugwara skrini ya mguso. Usitumie kamwe kalamu, penseli halisi, au kitu kingine chenye ncha kali kwenye skrini ya mguso.
Gusa na ushikilie ili kukokota kipengee
Weka kidole chako kwenye kipengee kwa sekunde chache, na utelezeshe kidole chako kwenye skrini.
Pitisha
Weka kidole chako kwenye skrini, na utelezeshe kidole chako kwenye mweleko unaotaka.
Tembeza kwenye orodha au menyu ndefu
Telezesha kidole chako kwa haraka katika mwelekeo wa juu au chini kwenye skrini, na uinue kidole chako. Ili kukomesha kutembeza, gusa skrini.
Kuza ndani au nje
Weka vidole 2 kwenye kipengee, kama vile ramani, picha, au ukurasa wavuti, na utelezeshe vidole vako vikiwa kando au pamoja.
Funga mwelekeo wa skrini
Skrini huzunguka kiotomatiki wakati unapindua simu kwa digrii 90.
Kufunga skrini katika hali ya wima, telezesha chini kutoka upande wa juu wa skrini, na uguse Zungusha kiotomatiki.
Rambaza kwa kutumia ishara
Kuwasha kwa kutumia urambazaji wa ishara, gusa Mipangilio > Mfumo > Ishara > Urambazaji wa mfumo > Urambazaji wa ishara.
Ili kuona programu zako zote, telezesha juu kuanzia chini ya skrini.
Ili kwenda kwenye skrini ya mwanzo, telezesha juu kutoka chini ya skrini. Programu uliyokuwa ukitumia hubakia imefunguliwa chinichini.
Kuona programu gani umefungua, telezesha juu kutoka chini ya skrini bila kutoa kidole chako hadi uone programu, kisha uondoe kidole chako.
Ili kubadilisha kwa programu nyingine iliyofunguliwa, gusa programu.
Ili kufunga programu zote zilizofunguliwa, telezesha kulia kupitia programu zote, na uguse FUTA ZOTE.
Ili urudi kwenye skrini ya awali ambayo ulikuwa unatumia, telezesha kutoka upande wa kulia au kushoto ya skrini. simu yako hukumbuka programu na tovuti zote ulizotembelea tangu wakati wa mwisho skrini yako ilipofungwa.
Rambaza kwa kutumia vitufe
Kuwasha vitufe vya urambazaji, gusa Mipangilio > Mfumo > Ishara > Urambazaji wa mfumo > Urambazaji wa vitufe 3.
Ili kuona programu zako zote, pitisha juu kwenye kitufe cha mwanzo fiber_manual_record.
IIi kwenda kwenye skrini ya mwanzo, gusa kitufe cha mwanzo. Programu uliyokuwa ukitumia hubakia imefunguliwa chinichini.
Ili kuona ni programu gani ulizofungua, gusa stop.
Ili kubadilisha kwa programu nyingine iliyofunguliwa, telezesha kulia na uguse programu.
Ili kufunga programu zote zilizofunguliwa, telezesha kulia kupitia programu zote, na uguse FUTA ZOTE.
Ili kurejesha kwenye skrini ya awali uliyokuwa, gusa . simu yako hukumbuka programu na tovuti zote ulizotembelea tangu wakati wa mwisho skrini yako ilipofungwa.
As we offer product user guides in many languages across different regions, you may be redirected to a Nokia phones web page outside of your selected location.
Contact the support team
Chat with us
Before starting chat with our customer support, please leave your contact details. Contact our chat support for online purchases support, product information, warranty support.
Prefer to bring your device in for our experts to have a look at? Find the location of your nearest Nokia & HMD phones, tablets and accessories care center.