Mwongozo wa mtumiaji wa Nokia XR21

Skip to main content
All Devices

Nokia XR21

Habari ya utoaji cheti

Maelezo ya Ufichuzi wa FCC RF

Kifaa hiki cha mkononi kinatimiza maelekezo yanayohusu ujiwekaji wazi kwa mawimbi ya redio kama yalivyowekwa na Tume ya Mawasiliano ya Serikali (FCC). Rejelea yafuatayo.

Kifaa chako cha mkononi ni transmita na kipokezi cha redio. Imeundwa na kutengenezwa ili kutozidisha vikomo vya utokezaji vya ufichuzi kwa nguvu ya frikwensi ya redio (RF) iliyowekwa na Tume ya Mawasiliano ya Serikali ya Serikali ya Marekani. Maelekezo haya yanategemea viwango ambavyo vimetengenezwa na shirika huru la kisayansi kupitia utathmini wa mara kwa mara na wa kina wa uchunguzi wa kisayansi. Viwango vinajumuisha viwango vikubwa vya usalama vilivyoundwa kuhakikisha usalama wa watu wote, Haijalishi umri na afya. Kiwango cha ufichuzi cha vifaa vya mkononi pasiwaya hutumia kizio cha vipimo kinachojulikana kama Kiwango Maalum cha Ufyonzaji au SAR. Kikomo cha SAR kilichowekwa na FCC ni 1.6 W/kg. Vipimo hutekelezwa katika mikao na maeneo (k.m. karibu na sikio na kuvaliwa kwenye mwili) kama inavyohitajika na FCC kwa kila modeli. Matumizi ya klipu za mshipi, vishikiliaji na vifaa vingine kama hivyo havipaswi kuwa na vijenzi vya chuma. Matumizi ya vifaa vya ziada ambavyo havitimizi mahitaji haya vinaweza kosa kutimiza mahitaji ya ufichuzi ya RF ya FCC, na vinapaswa kuepukwa. FCC imetoa Idhini ya Bidhaa kwa kifaa cha mkononi cha modeli hii ambacho viwango vyote vilivyoripotiwa vya SAR vimetathminiwa kuwa vinatii maelekezo ya utokezaji ya RF ya FCC. Maelezo ya ziada kuhusu Viwango Maalum vya Ufyonzaji (SAR) vinaweza kupatikana kwenye tovuti ya FCC ya www.fcc.gov/general/radio-frequency-safety-0. Kutuma data au ujumbe, muunganisho salama wa mtandao unahitajika. Utumaji unaweza kucheleweshwa hadi muunganisho huo upatikane. Fuata maagizo ya umbali wa kutenganisha hadi utumaji ukamilike. Wakati wa matumizi ya kawaida, thamani za SAR kwa kawaida huwa chini ya thamani zilizotajwa hapa juu. Hii ni kwa sababu, kwa malengo ya ubora wa mfumo na kupunguza mwingiliano kwenye mtandao, nguvu ya kufanya kazi ya kifaa chako cha mkononi hupunguzwa kiotomati wakati nguvu kamili haihitajiki kwa simu. Nguvu towe inavyoendelea kuwa chini, ndivyo thamani ya SAR inavyokuwa chini. Huenda modeli za vifaa zikawa na matoleo tofauti na zaidi ya thamani moja. Mabadiliko ya vijenzi na muundo yanaweza kufanyika baada ya muda na baadhi ya mabadiliko yanaweza kuathiri thamani za SAR. Kwa maelezo zaidi, nenda kwenye www.sar-tick.com. Kumbuka kwamba vifaa vya mkononi huenda vikapitisha hata kama hupigi simu. Kifaa chako cha mkononi kimeundwa pia kutimiza maelekezo ya Tume ya Mawasiliano ya Serikali ya Marekani (FCC). Tathmini za FCC za kifaa chako na maelezo zaidi kuhusu SAR yanaweza kupatikana kwenye http://transition.fcc.gov/oet/rfsafety/sar.html. Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kwamba maelezo ya sasa ya kisayansi hayaashirii hitaji la tahadhari zozote maalum wakati wa kutumia vifaa vya mkononi. Ikiwa unavutiwa na kupunguza ufichuzi wako, wanapendekeza upunguze matumizi yako au utumie kifaa kisichotumia mikono ili kuweka kifaa mbali na kichwa na mwili wako. Kwa maelezo zaidi na ufafanuzi na majadiliano kuhusu ufichuzi wa RF, nenda kwenye tovuti ya WHO kwenye https://www.who.int/health-topics/electromagnetic-fields#tab=tab_1.

Ilani ya FCC

Kifaa hiki kinatimiza sehemu ya 15 ya kanuni za FCC. Matumizi yanategemea hali mbili zifuatazo: (1) Huenda kifaa hiki kisisababishe mwingiliano mbaya, na (2) lazima kifaa hiki kikubali mwingiliano wowote uliopokea, ikiwa ni pamoja na mwingiliano ambao unaweza kusababisha matumizi yasiohitajika. Kwa maelezo zaidi, nenda kwenye www.fcc.gov/engineering-technology/electromagnetic-compatibility-division/radio-frequency-safety/faq/rf-safety. Mabadiliko au marekebisho yoyote yasioidhinishwa moja kwa moja na HMD Global yanaweza kubatilisha kibali cha kutumia kifaa hiki. Kumbuka: Kifaa hiki kimepimwa na kupatikana kutimiza vikwazo vya vifaa vya dijitali vya Ainisho B, kulingana na sheria ya 15 ya Kanuni za FCC. Vikwazo hivi vimeundwa ili kutoa kinga inayofaa dhidi ya mwingiliano mbaya katika maeneo ya makazi. Kifaa hiki huzalisha, kutumia na kinaweza kutoa miali ya nishati ya redio na, kama hakijawekwa na kutumika kulingana na maagizo, kinaweza kusababisha mwingiliano na mawasiliano ya redio. Hata hivyo, hakuna hakikisho kwamba mwingiliano hautafanyika katika uwekaji fulani. Ikiwa kifaa hiki hakitasababisha mwingiliano mbaya kwa mapokezi ya redio au runinga, ambayo inaweza kubainishwa kwa kuzima na kuwasha kifaa, mtumiaji anahimizwa kujaribu kusahihisha mwingiliano kwa hatua moja au zaidi ya zifuatazo:

  • Badilisha au weka antena ya kupokea mahali pengine.
  • Ongeza umbali kati ya kifaa na kipokezi.
  • Unganisha kifaa kwenye soketi tofauti na ile ambayo kipokezi kimeunganishwa.
  • Wasiliana na muuzaji au fundi mtaalamu wa redio/TV kwa usaidizi.

Kifaa hiki cha mkononi kinatimiza maelekezo yanayohusu ujiwekaji wazi kwa mawimbi ya redio.

Kifaa chako cha mkononi ni transmita na kipokezi cha redio. Kimeundwa kisizidishe viwango vya ufichuzi vya mawimbi ya redio (maeneo ya mawimbi ya redio ya sumaku ya umeme), vinavyopendekezwa na miongozo ya kimataifa kutoka kwa shirika huru la kisayansi ICNIRP. Maelekezo haya yanajumuisha viwango vya usalama vilivyoundwa kuhakikisha usalama wa watu wote, Haijalishi umri na afya. Maelekezo ya ufichuzi yanategemea Kiwango Maalum cha Ufyonzaji (SAR), ambacho ni onyesho la nguvu ya kiwango cha masafa ya redio (RF) ambayo inawekwa kichwani au mwilini wakati kifaa kinatumika. Kiwango cha SAR cha ICNIRP cha vifaa vya simu ni 2.0 W/kg kwa wastani wa gramu kumi za tishu.

Vipimo vya SAR vinatekelezwa kwa kifaa katika mikao ya kawaida ya uendeshaji, wakati kifaa kinapitisha katika kiwango chake cha juu zaidi kilichoidhinishwa cha nishati, katika bendi zote zilizopimwa za masafa.

Kifaa hiki kinatimiza matakwa ya maelekezo ya ujiwekaji wazi kichwani au wakati kimewekwa angalau inchi 5/8 (sentimita 1.5) kutoka kwenye mwili. Wakati kikasha cha kubebea, kishikiza kwenye mkanda au aina nyingi ya kishikizi kikitumika kwa matumizi ya kuvaliwa mwilini, kinatakiwa kisiwe na chuma na kinatakiwa kuweka angalia umbali uliotajwa hapo juu kutoka kwenye mwili.

Kutuma data au ujumbe, muunganisho salama wa mtandao unahitajika. Utumaji unaweza kucheleweshwa hadi muunganisho huo upatikane. Fuata maagizo ya umbali wa kutenganisha hadi utumaji ukamilike.

Wakati wa matumizi ya kawaida, thamani za SAR kwa kawaida huwa chini ya thamani zilizotajwa hapa juu. Hii ni kwa sababu, kwa malengo ya ubora wa mfumo na kupunguza mwingiliano kwenye mtandao, nguvu ya kufanya kazi ya kifaa chako cha mkononi hupunguzwa kiotomati wakati nguvu kamili haihitajiki kwa simu. Nguvu towe inavyoendelea kuwa chini, ndivyo thamani ya SAR inavyokuwa chini.

Huenda modeli za vifaa zikawa na matoleo tofauti na zaidi ya thamani moja. Mabadiliko ya vijenzi na muundo yanaweza kufanyika baada ya muda na baadhi ya mabadiliko yanaweza kuathiri thamani za SAR.

Kwa maelezo zaidi, nenda kwenye www.sar-tick.com. Kumbuka kwamba vifaa vya mkononi huenda vikapitisha hata kama hupigi simu.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kwamba maelezo ya sasa ya kisayansi hayaashirii hitaji la tahadhari zozote maalum wakati wa kutumia vifaa vya mkononi. Ikiwa unavutiwa na kupunguza ufichuzi wako, wanapendekeza upunguze matumizi yako au utumie kifaa kisichotumia mikono ili kuweka kifaa mbali na kichwa na mwili wako. Kwa maelezo zaidi na ufafanuzi na majadiliano kuhusu ufichuzi wa RF, nenda kwenye tovuti ya WHO kwenye www.who.int/health-topics/electromagnetic-fields#tab=tab_1.

Tafadhali rejelea www.hmd.com/sar kwa thamani ya juu ya SAR ya kifaa.

Did you find this helpful?
  • Sasisha simu yako
  • Vitufe na sehemu
  • Ingiza kadi za SIM
  • Chaji simu yako
  • Washa na usanidi simu yako
  • Tumia skrini ya mguso
  • Tumia eSIM yako
Maelezo ya bidhaa na usalama
  • Kwa usalama wako
  • Huduma za mtandao na gharama
  • Simu za dharura
  • Kuhudumia kifaa chako
  • Uchakataji upya
  • Alama ya pipa iliyo na mkato
  • Maelezo ya betri na chaja
  • Watoto wadogo
  • Vifaa vya matibabu
  • Vifaa vya matibabu vinavyopachikwa
  • Vifaa vya kusaidia kusikia
  • Linda mtoto wako dhidi ya vitu vyenye madhara
  • Magari
  • Mazingira yanayoweza kulipuka
  • Habari ya utoaji cheti
  • Kuhusu Usimamizi wa haki za Dijitali
  • Hakimiliki na ilani nyingine

Useful Links

PDFSoftware UpdatesFull SpecificationsEnvironmental Profile

Countries and Languages

As we offer product user guides in many languages across different regions, you may be redirected to a Nokia phones web page outside of your selected location.

Countries and Languages

Choose Language

Contact the support team

Chat with us

Before starting chat with our customer support, please leave your contact details. Contact our chat support for online purchases support, product information, warranty support.

Start chat

Chat with us

Before starting chat with our customer support, please leave your contact details. Contact our chat support for online purchases support, product information, warranty support.

Fields marked with an asterisk are mandatory.

Your personal data will be processed according to HMD Global’s Privacy Policy and the HMD Support Supplement.

Email us

Tell us about your problem and we'll get back to you via email.

Contact us

Care centers

Prefer to bring your device in for our experts to have a look at? Find the location of your nearest Nokia & HMD phones, tablets and accessories care center.

Find a care center near you