Ikiwa kumbukumbu ya simu inajaa, kwanza kagua na uondoe vitu usivyovihitaji tena:
Badala ya kuondoa, unaweza pia kusogeza faili kwenye kadi ya kumbukumbu.
Ubora wa kadi ya kumbukumbu unaweza kuathiri utendakazi wa simu yako pakubwa. Ili uweze kunufaika zaidi na simu yako, tumia kadi ya 4–128GB kutoka kwa mtengenezaji anayefahamika.
Tumia tu kadi za kumbukumbu zinazotangamana zilizoidhinishwa kutumiwa na kifaa hiki. Kadi zisizotangamana zinaweza kuharibu kadi na kifaa na kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Huwezi kufuta baadhi ya programu ambazo zilisakinishwa mapema kwenye kifaa chako. Lakini unaweza kuzilemaza na zitafichwa kutoka kwenye orodha ya programu kwenye kifaa chako. Ukilemaza programu, unaweza kuiongeza kwenye kifaa chako.
Ikiwa programu iliyosakinishwa inategemea programu iliyotolewa, programu iliyosakinishwa inaweza koma kufanya kazi. Kwa maelezo, angalia nyaraka za mtumiaji kwenye programu iliyosakinishwa.
Unaweza kuongeza programu iliyolemazwa kwenye orodha ya programu.
Unaweza kunakili picha, video, na maudhui mengine yaliyoundwa na wewe kati ya simu na kompyuta yako ili kuonyesha au kuzihifadhi.
Hakikisha umeweka faili katika folda sahihi kwenye simu yako, au huenda usiweze kuziona.
Before starting chat with our customer support, please leave your contact details. Contact our chat support for online purchases support, product information, warranty support.
Start chatPrefer to bring your device in for our experts to have a look at? Find the location of your nearest Nokia & HMD phones, tablets and accessories care center.
Find a care center near you