Mwongozo wa mtumiaji wa Nokia 2660 Flip

Skip to main content
All Devices

Nokia 2660 Flip

Hakimiliki na ilani nyingine

Hakimiliki

Upatikanaji wa bidhaa, vipengele, programu na huduma unaweza kutofautiana kimaeneo. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na mchuuzi au mtoa huduma wako. Kifaa hiki kinaweza kuwa na bidhaa, teknolojia au programu ambayo inategemea sheria na masharti ya usafirishaji nje ya nchi kutoka Marekani na nchi nyingine. Uchepushaji kinyume na sheria ni marufuku.

Yaliyomo katika waraka huu yametolewa "kama yalivyo". Isipokuwa kama inatakiwa hivyo na sheria husika, hakuna dhamana za aina yoyote, ama za moja kwa moja au zisizo bayana, pamoja na, lakini isiyokomea hapo, dhamana zisizo bayana za uuzikaji wa kibiashara na ufaaji kwa matumizi fulani, zinazotolewa kuhusiana na usahihi, uaminikaji au yaliyomo ndani ya waraka huu. HMD Global ina haki ya kupitia na kusahihisha waraka huu au kuuondoa wakati wowote bila kutoa taarifa kwanza.

Kwa kadiri inayohusiwa na sheria husika, hakuna wakati wowote ule HMD Global au wenye leseni wake watawajibika kwa upotevu wowote wa data au mapato au uharibifu wowote ule, uwe maalum, wa ajali, unatokana na, au usiokuwa wa moja kwa moja uliosababishwa.

Ni marufuku kutoa upya, kuhamisha au kusambaza sehemu ya yaliyomo au yote katika waraka huu katika hali yoyote ile bila ya kupewa kwanza idhini ya kuandikwa kutoka kwa HMD Global. HMD Global inaendesha sera ya kuendelea kubuni. HMD Global ina haki ya kufanya mabadiliko na kuboresha bidhaa yake yoyote iliyoelezwa katika waraka huu bila kutoa taarifa kwanza.

HMD Global haitoi uhakikisho wowote, waranti au kuwajibika kwa utendakazi, maudhui, au usaidizi wa mtumiaji wa programu za mhusika mwingine zilizotolewa na kifaa chako. Kwa kutumia programu, unakubali kwamba programu imetolewa kama ilivyo.

Upakuaji wa ramani, michezo, muziki na video na upakiaji wa picha na video huenda ukajumuisha upitishaji wa viwango vikubwa vya data. Huenda mtoa huduma wako akatoza kwa upitishaji data. Upatikanaji wa bidhaa, huduma na vipengele fulani unaweza zikatofautiana kimaeneo. Tafadhali wasiliana na muuzaji wa eneo lako kwa maelezo zaidi na upatikanaji wa chaguo za lugha.

Vipengele, utendakazi na ainisho nyingine za bidhaa zinaweza kutegemea mtandao na hutegemea masharti, sheria, na gharama za ziada.

Ainisho, vipengele na maelezo mengine yote ya bidhaa yaliyotolewa yanaweza kubadilika bila ilani.

Sera ya Faragha ya HMD Global, inapatikana kwenye http://www.hmd.com/privacy, hutumika kwa matumizi yako ya kifaa.

HMD Global Oy ndio ina leseni ya kipekee ya chapa ya Nokia ya simu na kompyuta kibao. Nokia ni alama ya biashara iliyosajiliwa ya Nokia Corporation.

Alama ya neno na nembo za Bluetooth zinamilikiwa na Bluetooth SIG, Inc. na matumizi yoyote ya alama hizo na HMD Global yako chini ya leseni.

Bidhaa hii inajumuisha programu huria. Kwa hakimiliki husika na ilani, vibali, na ukubalifu mwingine, chagua *#6774# kwenye skrini ya mwanzo.

Did you find this helpful?
  • Vitufe na sehemu
  • Sanidi na uwashe simu yako
  • Chaji simu yako
  • Vitufe
Maelezo ya bidhaa na usalama
  • Kwa usalama wako
  • Simu za dharura
  • Kuhudumia kifaa chako
  • Uchakataji upya
  • Alama ya pipa iliyo na mkato
  • Maelezo ya betri na chaja
  • Watoto wadogo
  • Vifaa vya matibabu
  • Vifaa vya matibabu vinavyopachikwa
  • Vifaa vya kusaidia kusikia
  • Linda kifaa chako dhidi ya maudhui mabaya
  • Magari
  • Mazingira yanayoweza kulipuka
  • Habari ya utoaji cheti
  • Kuhusu Usimamizi wa haki za Dijitali
  • Hakimiliki na ilani nyingine
  • Online safety

Useful Links

PDFSoftware UpdatesFull SpecificationsEnvironmental Profile

Countries and Languages

As we offer product user guides in many languages across different regions, you may be redirected to a Nokia phones web page outside of your selected location.

Countries and Languages

Choose Language

Contact the support team

Chat with us

Before starting chat with our customer support, please leave your contact details. Contact our chat support for online purchases support, product information, warranty support.

Start chat

Chat with us

Before starting chat with our customer support, please leave your contact details. Contact our chat support for online purchases support, product information, warranty support.

Fields marked with an asterisk are mandatory.

Your personal data will be processed according to HMD Global’s Privacy Policy and the HMD Support Supplement.

Email us

Tell us about your problem and we'll get back to you via email.

Contact us

Care centers

Prefer to bring your device in for our experts to have a look at? Find the location of your nearest Nokia & HMD phones, tablets and accessories care center.

Find a care center near you