Mwongozo wa mtumiaji wa Nokia T21

Skip to main content
All Devices

Nokia T21

Hakimiliki na ilani nyingine

Hakimiliki na ilani nyingine

Upatikani wa baadhi ya bidhaa, vipengele, programu na huduma zilizofafanuliwa katika mwongozo huu zinaweza kutofautiana kulingana na eneo na uhitaji uamilishaji, kujisajili, mtandao na/au muunganisho wa intaneti na mpango unaofaa wa huduma. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na mchuuzi au mtoa huduma wako. Kifaa hiki kinaweza kuwa na bidhaa, teknolojia au programu ambayo inaathiriwa na sheria na kanuni za usafirishaji nje ya nchi kutoka Marekani na nchi nyingine. Uchepushaji kinyume na sheria ni marufuku.

Yaliyomo katika waraka huu yametolewa "kama yalivyo". Isipokuwa kama inatakiwa hivyo na sheria husika, hakuna dhamana za aina yoyote, ama za moja kwa moja au zisizo bayana, pamoja na, lakini isiyokomea hapo, dhamana zisizo bayana za uuzikaji wa kibiashara na ufaaji kwa matumizi fulani, zinazotolewa kuhusiana na usahihi, uaminikaji au yaliyomo ndani ya waraka huu. HMD Global ina haki ya kupitia na kusahihisha waraka huu au kuuondoa wakati wowote bila kutoa taarifa kwanza.

Kwa kadiri inayohusiwa na sheria husika, hakuna wakati wowote ule HMD Global au wenye leseni wake watawajibika kwa upotevu wowote wa data au mapato au uharibifu wowote ule, uwe maalum, wa ajali, unatokana na, au usiokuwa wa moja kwa moja uliosababishwa.

Ni marufuku kutoa upya, kuhamisha au kusambaza sehemu ya yaliyomo au yote katika waraka huu katika hali yoyote ile bila ya kupewa kwanza idhini ya kuandikwa kutoka kwa HMD Global. HMD Global inaendesha sera ya kuendelea kubuni. HMD Global ina haki ya kufanya mabadiliko na kuboresha bidhaa yake yoyote iliyoelezwa katika waraka huu bila kutoa taarifa kwanza.

HMD Global haitoi wakilishi wowote, waranti au kuwajibika kwa utendaji kazi, maudhui, au usaidizi wa mtumiaji wa programu za mhusika wa tatu zilizotolewa na kifaa chako. Kwa kutumia programu, unakubali kwamba programu imetolewa kama ilivyo.

Upakuaji wa ramani, michezo, muziki na video na upakiaji taswira na video huenda ukajumuisha upitishaji wa viwango vikubwa vya data. Huenda mtoa huduma wako akatoza kwa upitishaji data. Upatikanaji wa bidhaa, huduma na vipengele fulani unaweza zikatofautiana kimaeneo. Tafadhali wasiliana na muuzaji wa eneo lako kwa maelezo zaidi na upatikanaji wa chaguo za lugha.

Vipengele, utendakazi na ainisho nyingine za bidhaa zinaweza kutegemea mtandao na hutegemea masharti, sheria, na gharama za ziada.

Ainisho, vipengele na maelezo mengine yote ya bidhaa yaliyotolewa yanaweza kubadilika bila ilani.

Sera ya Faragha ya HMD Global, inapatikana kwenye http://www.hmd.com/privacy, hutumika kwa matumizi yako ya kifaa.

HMD Global Oy ndio ina leseni ya kipekee ya chapa ya Nokia ya simu na kompyuta kibao. Nokia ni alama ya biashara iliyosajiliwa ya Nokia Corporation.

Google na alama na nembo nyingine husiani ni alama za biashara za Google LLC.

Alama ya neno na nembo za Bluetooth zinamilikiwa na Bluetooth SIG, Inc. na matumizi yoyote ya alama hizo na HMD Global yako chini ya leseni.

Tumia Hali ya mwanga wa chini wa bluu

Tumia Hali ya mwanga wa chini wa bluu

Mwanga wa bluu ni rangi katika spektra inayoonekana ya mwanga ambayo inaweza kuonekana kwa macho ya binadamu. Kati ya rangi zote ambazo macho ya binadamu inatambua (urujuani, nili, bluu, kijani, manjano, chungwa, nyekundu), bluu ndio ina masafa mafupi zaidi na kwa hivyo huzalisha kiwango cha juu zaidi cha kawi. Kwa kuwa mwangaza wa bluu hupita kwenye konea na lensi ya macho yako kabla ya kufikia retina, unaweza kusababisha, kwa mfano, kuwashwa na macho mekundu, maumivu ya kichwa, kutoona vizuri, na kutolala vizuri. Ili kuzuia na kupunguza mwangaza wa bluu, sekta ya skrini imetengeneza suluhu kama vile Hali ya mwanga wa chini wa bluu. Ili kuwasha Hali ya mwanga wa chini wa bluu kwenye kompyuta kibao yako, gusa Mipangilio > Skrini > Mwanga wa Usiku > Washa. Ikiwa unataka kuangalia skrini ya kompyuta kibao yako kwa muda mrefu, pumzika mara kwa mara na utulize macho yako kwa kuangalia vitu vilivyo mbali.

OZO

OZO

OZO ni alama ya biashara Nokia Technologies Oy.

Did you find this helpful?
  • Vitufe na sehemu
  • Ingiza SIM na kadi za kumbukumbu
  • Chaji kompyuta kibao yako
  • Washa na usanidi kompyuta kibao yako
  • Funga au fungua kompyuta kibao yako
  • Tumia skrini ya mguso
Maelezo ya bidhaa na usalama
  • Kwa usalama wako
  • Huduma za mtandao na gharama
  • Kuhudumia kifaa chako
  • Uchakataji upya
  • Alama ya pipa iliyo na mkato
  • Maelezo ya betri na chaja
  • Watoto wadogo
  • Vifaa vya matibabu
  • Vifaa vya matibabu vinavyopachikwa
  • Vifaa vya kusaidia kusikia
  • Linda mtoto wako dhidi ya vitu vyenye madhara
  • Magari
  • Mazingira yanayoweza kulipuka
  • Habari ya utoaji cheti
  • Kuhusu Usimamizi wa haki za Dijitali
  • Hakimiliki na ilani nyingine

Useful Links

PDFSoftware UpdatesFull SpecificationsEnvironmental Profile

Countries and Languages

As we offer product user guides in many languages across different regions, you may be redirected to a Nokia phones web page outside of your selected location.

Countries and Languages

Choose Language

Contact the support team

Chat with us

Before starting chat with our customer support, please leave your contact details. Contact our chat support for online purchases support, product information, warranty support.

Start chat

Chat with us

Before starting chat with our customer support, please leave your contact details. Contact our chat support for online purchases support, product information, warranty support.

Fields marked with an asterisk are mandatory.

Your personal data will be processed according to HMD Global’s Privacy Policy and the HMD Support Supplement.

Email us

Tell us about your problem and we'll get back to you via email.

Contact us

Care centers

Prefer to bring your device in for our experts to have a look at? Find the location of your nearest Nokia & HMD phones, tablets and accessories care center.

Find a care center near you