Mwongozo wa mtumiaji wa Nokia 6.2

Skip to main content
All Devices

Nokia 6.2

NFC

Chunguza ulimwengu karibu na wewe. Ikiwa simu yako inakubali Mawasiliano ya Karibu na Eneo (NFC), unaweza kugusa vifaa vya ziada ili kuviunganisha, na uguse lebo ili kumpigia mtu simu au kufungua tovuti. Utendaji wa NFC unaweza kutumika na huduma na teknolojia fulani kama gusa ili kulipa kwa kutumia kifaa chako. Huduma hizi zinaweza kukosa kupatikana katika eneo wako. Kupata maelezo zaidi kuhusu upatikanaji wa huduma hizi, wasiliana na mtoa huduma wa mtandao wako.

Anza Kutumia NFC

Washa vipengele vya NFC kwenye simu yako, na uanze kugusa ili kushiriki vitu au kuunganisha kwenye vifaa. Ili kuona kama simu yako inakubali NFC, gusa Mipangilio > Vifaa vilivyounganishwa > Mapendeleo ya Muunganisho.

Ukiwa na NFC, unaweza:

  • Unganisha kwenye vifaa vya ziada vinavyotangamana vya Bluetooth ambavyo vinakubali NFC, kama vile vifaa vya sauti au kipasa sauti pasi waya.
  • Gusa lebo ili upate maudhui zaidi ya simu yako, au kufikia huduma za mtandaoni.
  • Lipa kwa kutumia simu yako, ikiwa inakubaliwa na mtoa huduma wa mtandao wako.

Eneo la NFC liko nyuma ya simu yako. Gusa simu, vifaa vya simu, lebo, au visomaji vingine na eneo la NFC.

  1. Gusa Mipangilio > Vifaa vilivyounganishwa > Mapendeleo ya muunganisho > NFC.
  2. Washa NFC.

Kabla ya kutumia NFC, hakikisha skrini na vitufe vimefungwa.

Soma lebo za NFC

Lebo za NFC zinaweza kuwa na maelezo, kama vile anwani ya wavuti, nambari ya simu, au kadi ya biashara. Maelezo unayotaka yako umbali wa mguso tu.

Ili kusoma lebo. gusa lebo na eneo la NFC ya simu yako.

Kumbuka: Malipo na programu na huduma za tikiti zinatolewa na wahusika wengine. HMD Global haitoi waranti yoyote au kuwajibika kwa programu au huduma zozote kama hizo ikiwemo usaidizi, utendakazi, miamala, au upotezaji wa thamani ya kipesa. Huenda ukahitaji kusakinisha upya na kuamilisha kadi ulizoongeza na hata pia programu ya malipo au tikiti baada ya kifaa chako kukarabatiwa.

Unganisha kwenye kifaa cha ziada cha Bluetooth na NFC

Unatumia mikono yako? Tumia vifaa vya sauti. Au kwa nini usisikilize muziki kwa kutumia vipasa sauti pasi waya? Unahitaji tu kugusa kifaa cha ziada kinachotangaman na simu yako.

  1. Gusa eneo la NFC na kifaa cha ziada na eneo la NFC ya simu yako.*
  2. Fuata maagizo kwenye skrini.

*Vifaa vya ziada vinauzwa kando. Upatikanaji wa vifaa vya ziada hutofautiana kimaeneo.

Tenganisha kifaa cha ziada kilichounganishwa

Ikiwa hutaki kuunganishwa tena kwenye kifaa cha ziada, unaweza kutenganisha kifaa hicho cha ziada.

Gusa tena eneo la NFC la kifaa cha ziada.

Kwa maelezo zaidi, angalia mwongozo wa mtumiaji wa kifaa cha ziada.

Did you find this helpful?
  • Sasisha simu yako
  • Vitufe na sehemu
  • Ingiza SIM na kadi ya kumbukumbu
  • Chaji simu yako
  • Washa na usanidi simu yako
  • Mipangilio ya SIM Mbili
  • Funga au fungua simu yako
  • Tumia skrini ya mguso
Intaneti na miunganisho
  • Amilisha Wi-Fi
  • Tumia muunganisho wa data ya simu
  • Vinjari wavuti
  • Bluetooth®
  • NFC
  • VPN

Useful Links

PDFSoftware Updates

Countries and Languages

As we offer product user guides in many languages across different regions, you may be redirected to a Nokia phones web page outside of your selected location.

Countries and Languages

Choose Language

Contact the support team

Chat with us

Before starting chat with our customer support, please leave your contact details. Contact our chat support for online purchases support, product information, warranty support.

Start chat

Chat with us

Before starting chat with our customer support, please leave your contact details. Contact our chat support for online purchases support, product information, warranty support.

Fields marked with an asterisk are mandatory.

Your personal data will be processed according to HMD Global’s Privacy Policy and the HMD Support Supplement.

Email us

Tell us about your problem and we'll get back to you via email.

Contact us

Care centers

Prefer to bring your device in for our experts to have a look at? Find the location of your nearest Nokia & HMD phones, tablets and accessories care center.

Find a care center near you