Ikiwa simu yako inakubali Mawasiliano ya Karibu na Eneo (NFC), unaweza kugusa vifaa vya ziada ili kuviunganisha, na uguse lebo ili kumpigia mtu simu au kufungua tovuti. Utendaji wa NFC unaweza kutumika na huduma na teknolojia fulani kama gusa ili kulipa kwa kutumia kifaa chako. Huduma hizi zinaweza kukosa kupatikana katika eneo wako. Kupata maelezo zaidi kuhusu upatikanaji wa huduma hizi, wasiliana na mtoa huduma wa mtandao wako.
Kabla ya kutumia NFC, hakikisha skrini na vitufe vimefungwa.
Eneo la NFC liko nyuma ya simu yako.
Ili uunganishe simu yako kwenye simu nyingine au kifaa cha ziada, au kusoma lebo za NFC, gusa tu kwenye kifaa kingine au gusa eneo la NFC la simu yako.
Kumbuka: Malipo na programu na huduma za tikiti zinatolewa na wahusika wengine. HMD Global haitoi waranti yoyote au kuwajibika kwa programu au huduma zozote kama hizo ikiwemo usaidizi, utendakazi, miamala, au upotezaji wa thamani ya kipesa. Huenda ukahitaji kusakinisha upya na kuamilisha kadi ulizoongeza na hata pia programu ya malipo au tikiti baada ya kifaa chako kukarabatiwa.
Ikiwa hutaki kuunganishwa tena kwenye kifaa cha ziada, unaweza kutenganisha kifaa hicho cha ziada.
Gusa tena eneo la NFC la kifaa cha ziada.
Kwa maelezo zaidi, angalia mwongozo wa mtumiaji wa kifaa cha ziada.