
Fungua macho yako na uhakikishe uso wako unaonekana kikamilifu na hujafunikwa na kitu chochote, kama vile kofia au miwani.
Kumbuka: Kutumia uso wako kufungua simu yako si salama kama kutumia alama ya kidole, ruwaza au nenosiri. Huenda simu yako imefunguliwa na mtu au kitu chenye mwonekano huo mmoja. Huenda kufungua kwa uso kusifanye kazi vizuri katika mazingira yenye mwangaza wa nyuma au wenye giza au mkali.
Ili kufungua simu yako, washa skrini yako na uangalie kamera ya mbele.
Ikiwa kuna hitilafu ya kutambua uso, na huwezi kutumia mbinu mbadala za kuingia ili kurejesha au kuweka upya simu kwa njia yoyote ile, simu yako itahitaji huduma. Huenda gharama ya ziada ikatumika, na data yote ya kibinafsi kwenye simu huenda ikafutwa. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na kituo cha huduma kilichoidhinishwa kilicho karibu cha simu yako, au muuzaji wa simu yako.