Nokia X71 user guide

Skip to main content
All Devices

Nokia X71

Misimbo ya ufikiaji

Jifunze misimbo tofauti kwenye simu yako ni ya nini.

Msimbo wa PIN au PIN2

Misimbo ya PIN au PIN2 ina dijiti 4-8.

Misimbo hii hulinda SIM kadi yako dhidi ya matumizi yasioidhinishwa au huhitajika ili kufikia vipengee vingine. Unaweza kuweka simu yako kukuuliza msimbo wa PIN wakati unapoiwasha.

Ukisahau misimbo au iwe haijatolewa pamoja na kadi yako, wasiliana na mtoa huduma wa mtandao wako.

Ukicharaza msimbo vibaya mara 3 zikifuatana, unahitaji kufungua msimbo kwa kutumia msimbo wa PUK au PUK2.

Misimbo ya PUK au PUK2

Misimbo ya PUK au PUK2 zinahitajika ili kufungua msimbo wa PIN au PIN2.

Ikiwa misimbo haijatolewa na SIM kadi yako, wasiliana na mtoa huduma wako wa mtandao.

Msimbo wa kufunga

Msimbo wa kufunga unajulikana pia kama msimbo au nenosiri la usalama.

Msimbo wa kufunga hukusaidia kulinda simu yako dhidi ya matumizi yasiyoidhinishwa. Unaweza kuweka simu yako kukuuliza msimbo wa kufunga ambao unafasili. Weka msimbo kuwa siri na mahali salama, kando na simu yako.

Ukisahau msimbo na simu yako imefungwa, simu yako itahitaji huduma. Huenda gharama ya ziada ikatumika, na data yote ya kibinafsi kwenye simu huenda ikafutwa. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na kituo cha huduma kilichoidhinishwa kilicho karibu cha simu yako, au muuzaji wa simu yako.

Msimbo wa IMEI

Msimbo wa IMEI hutumiwa kutambua simu katika mtandao. Huenda pia ukahitaji kupeana nambari kwa kituo chako kilichoidhinishwa cha huduma au muuzaji wa simu.

Ili kuona nambari yako ya IMEI, piga *#06#.

Msimbo wa IMEI wa simu yako umechapishwa pia kwenye simu yako au kwenye trei ya SIM kulingana na modeli ya simu yako. Ikiwa simu yako ina kifuniko kinachoweza kuondolewa cha nyuma, unaweza kupata msimbo wa IMEI chini ya kifuniko.

IMEI inaweza kuonekana pia kwenye kisanduku halisi cha mauzo.

Tafuta au funga simu yako

Ukipoteza simu yako, unaweza kuitafuta, kuifunga, au kuifuta kwa mbali ikiwa umeingia kwenye Akaunti ya Google. Tafuta Kifaa Changu huwashwa kimsingi kwa simu zinazohusishwa na Akaunti ya Google.

Ili utumie Tafuta Kifaa Changu, lazima simu yako iwe:

  • Imewashwa
  • Umeingia kwenye Akaunti ya Google
  • Imeunganishwa kwenye data ya simu au Wi-Fi
  • Inapatika kwenye Google Play
  • Eneo limewashwa
  • Tafuta Kifaa Changu imewashwa

Wakati Tafuta Kifaa Changu kinapounganishwa na simu yako, utaona eneo la simu, na simu itapata arifa.

  1. Fungua android.com/find kwenye kompyuta, kompyuta kibao au simu iliyounganishwa kwenye intaneti na uingie kwenye Akaunti yako ya Google.
  2. Ikiwa una zaidi ya simu moja, bofya simu iliyopotea juu ya skrini.
  3. Kwenye ramani, angalia kuhusu mahali simu iko. Eneo huwa ukadiriaji na huenda lisiwe sahihi.

Iwapo kifaa chako hakiwezi kupatikana, Tafuta Kifaa Changu itaonyesha eneo la mwisho linalojulikana, ikiwa ipo. Ili kufunga au kufuta simu yako, fuata maagizo kwenye tovuti.

Did you find this helpful?
  • Sasisha simu yako
  • Vitufe na sehemu
  • Ingiza au ondoa SIM na kadi ya kumbukumbu
  • Chaji simu yako
  • Washa na usanidi simu yako
  • Dual SIM settings
  • Kuweka ID ya alama ya kidole
  • Funga au fungua simu yako
  • Tumia skrini ya mguso
Linda simu yako
  • Linda simu yako kwa kutumia alama ya kidole chako
  • Badilisha msimbo wako wa PIN ya SIM
  • Misimbo ya ufikiaji

Useful Links

PDFSoftware Updates

Countries and Languages

Contact the support team

Chat with us

Before starting chat with our customer support, please leave your contact details. Contact our chat support for online purchases support, product information, warranty support.

Start chat

Chat with us

Before starting chat with our customer support, please leave your contact details. Contact our chat support for online purchases support, product information, warranty support.

Fields marked with an asterisk are mandatory.

Your personal data will be processed according to HMD Global’s Privacy Policy and the HMD Support Supplement.

Email us

Tell us about your problem and we'll get back to you via email.

Contact us

Care centers

Prefer to bring your device in for our experts to have a look at? Find the location of your nearest Nokia & HMD phones, tablets and accessories care center.

Find a care center near you