Nokia X71 user guide

Skip to main content
All Devices

Nokia X71

Hifadhi

Ili kukagua kiwango cha kumbukumbu kinachopatikana, gusa Mipangilio > Hifadhi.

Kagua kumbukumbu inayopatikana kwenye simu yako

Ikiwa kumbukumbu ya simu inajaa, kwanza kagua na uondoe vitu usivyovihitaji tena:

  • Maandishi, medianuwai, na ujumbe wa barua
  • Ingizo na maelezo ya majina
  • Programu
  • Muziki, picha, au video

Badala ya kuondoa, unaweza pia kusogeza faili kwenye kadi ya kumbukumbu.

Ubora wa kadi ya kumbukumbu unaweza kuathiri utendakazi wa simu yako pakubwa. Ili uweze kunufaika zaidi na simu yako, tumia kadi ya 4–128GB kutoka kwa mtengenezaji anayefahamika.

Tumia tu kadi za kumbukumbu zinazotangamana zilizoidhinishwa kutumiwa na kifaa hiki. Kadi zisizotangamana zinaweza kuharibu kadi na kifaa na kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.

Ili kukagua kiasi cha kumbukumbu unacho na jinsi inavyotumika, gusa Mipangilio > Hifadhi.

Ondoa programu zilizopakuliwa

Gusa Play Store > menu > Programu na michezo yangu, chagua programu unayotaka kuondoa, na uguse SANIDUA.

Zima programu

Huwezi kufuta baadhi ya programu ambazo zilisakinishwa mapema kwenye kifaa chako. Lakini unaweza kuzilemaza na zitafichwa kutoka kwenye orodha ya programu kwenye kifaa chako. Ukilemaza programu, unaweza kuiongeza kwenye kifaa chako.

  1. Gusa Mipangilio > Programu na arifa.
  2. Gusa jina la programu.
  3. Gusa ZIMA. Huenda usiweze kulemaza programu zote.

Ikiwa programu iliyosakinishwa inategemea programu iliyotolewa, programu iliyosakinishwa inaweza koma kufanya kazi. Kwa maelezo, angalia nyaraka za mtumiaji kwenye programu iliyosakinishwa.

Rejesha programu iliyolemazwa

Unaweza kuongeza programu iliyolemazwa kwenye orodha ya programu.

  1. Gusa Mipangilio > Programu na arifa.
  2. Gusa jina la programu.
  3. Gusa WASHA.

Nakili maudhui kati ya simu yako na kompyuta

Unaweza kunakili picha, video, na maudhui mengine yaliyoundwa na wewe kati ya simu na kompyuta yako ili kuonyesha au kuzihifadhi.

  1. Unganisha simu yako kwenye kompyuta inayotangamana na kebo ya USB inayotangamana.
  2. Kwenye kompyuta yako, fungua kisimamia faili, na uvinjari kwenye simu yako.
  3. Kokota na udondoshe vipengee kutoka kwenye simu hadi kompyuta yako, au kutoka kwenye kompyuta hadi simu yako.

Hakikisha umeweka faili katika folda sahihi kwenye simu yako, au huenda usiweze kuziona.

Did you find this helpful?
  • Sasisha simu yako
  • Vitufe na sehemu
  • Ingiza au ondoa SIM na kadi ya kumbukumbu
  • Chaji simu yako
  • Washa na usanidi simu yako
  • Dual SIM settings
  • Kuweka ID ya alama ya kidole
  • Funga au fungua simu yako
  • Tumia skrini ya mguso
Visasisho na hifadhi nakala za programu
  • Sasisha programu ya simu yako
  • Hifadhi nakala ya data yako
  • Rejesha mipangilio halisi na uondoe maudhui binafsi kwenye simu yako
  • Hifadhi

Useful Links

PDFSoftware Updates

Countries and Languages

Contact the support team

Chat with us

Before starting chat with our customer support, please leave your contact details. Contact our chat support for online purchases support, product information, warranty support.

Start chat

Chat with us

Before starting chat with our customer support, please leave your contact details. Contact our chat support for online purchases support, product information, warranty support.

Fields marked with an asterisk are mandatory.

Your personal data will be processed according to HMD Global’s Privacy Policy and the HMD Support Supplement.

Email us

Tell us about your problem and we'll get back to you via email.

Contact us

Care centers

Prefer to bring your device in for our experts to have a look at? Find the location of your nearest Nokia & HMD phones, tablets and accessories care center.

Find a care center near you