Nokia X71 user guide

Skip to main content
All Devices

Nokia X71

Andika maandishi

Jifunze jinsi ya kuandika maandishi kwa haraka na vizuri kwa kutumia kibodi ya simu yako.

Tumia kibodi kwenye skrini

Kuandika kwa kutumia kibodi kwenye skrini ni rahisi. Unaweza kutumia kibodi ukiwa umeshikilia simu yako katika hali wima au mlalo. Mpangilio wa kibodi unaweza kutofautiana katika programu na lugha tofauti.

Ili kufungua kibodi kwenye skrini, gusa kisanduku cha maandishi.

Badilisha kati ya vibambo vikubwa na vidogo

Gusa kitufe cha shift. Ili kuwasha hali ya caps lock, gusa kitufe mara mbili. Ili kurejea hali ya kawaida, gusa tena kitufe cha shift.

Charaza namba au kibambo maalum

Gusa nambari na Kitufe cha alama. Baadhi vitufe vya vibambo maalum huleta alama zaidi. Ili kuona alama zaidi, gusa na ushikilie alama au kibambo maalum.

Ingiza emoji

Gusa kitufe cha emoji, na uchague emoji.

Nakili au bandika maandishi

Gusa na ushikilie neno, kokota viweka alama kabla na baada ya neno ili kuangazia sehemu unayotaka kunakili na uguse NAKILI. Ili kubandika maandishi, gusa ni wapi unataka kubandika maandishi na uchague BANDIKA.

Ongeza lafudhi kwa kibambo

Gusa na ushikilie kibambo, na uguse lafudhi au kibambo cha lafushi, ikiwa inakubaliwa na kibodi yako.

Futa kibambo

Gusa kitufe cha backspace.

Sogeza kasa

Ili kuhariri neno uliloandika, gusa neno, na uburute kasa mahali unapoitaka.

Tumia mapendekezo ya neno la kibodi

Simu yako hupendekeza maneno unapokuwa ukiandika, ili kukusaidia kuandika kwa haraka na kwa usahihi zaidi. Mapendekezo ya maneno yanaweza kutopatikana katika lugha zote.

Wakati unapoanza kuandika neno, simu yako itapendekeza maneno yanayowezekana. Neno unalotaka likionyeshwa kwenye upau wa mapendekezo, chagua neno. Ili kuona mapendekezo zaidi, gusa na ushikilie pendekezo.

Dokezo: Ikiwa neno lililopendekezwa limewekwa alama ya koza, simu huitumia kiotomatiki ili kubadilisha neno uliloandika. Ikiwa neno si sahihi, gusa na ushikilie ili kuona mapendekezo mengine machache.

Ikiwa hutaki kibodi kupendekeza maneno unapokuwa ukicharaza, zima sahihisho za matini. Gusa Mipangilio > Mfumo > Lugha na ingizo > Kibodi pepe. Teua kibodi unayotumia kwa kawaida. Gusa Usahihishaji matini na uzime mbinu za kusahihisha matini ambayo hutaki kutumia.

Did you find this helpful?
  • Sasisha simu yako
  • Vitufe na sehemu
  • Ingiza au ondoa SIM na kadi ya kumbukumbu
  • Chaji simu yako
  • Washa na usanidi simu yako
  • Dual SIM settings
  • Kuweka ID ya alama ya kidole
  • Funga au fungua simu yako
  • Tumia skrini ya mguso
Misingi
  • Binafsisha simu yako
  • Fungua na ufunge programu
  • Arifa
  • Dhibiti sauti
  • Picha za skrini
  • Maisha ya betri
  • Okoa gharama ya utumiaji data nje ya mtandao wako wa kawaida
  • Andika maandishi
  • Tarehe na saa
  • Kalenda
  • Saa na kengele
  • Ufikiaji

Useful Links

PDFSoftware Updates

Countries and Languages

Contact the support team

Chat with us

Before starting chat with our customer support, please leave your contact details. Contact our chat support for online purchases support, product information, warranty support.

Start chat

Chat with us

Before starting chat with our customer support, please leave your contact details. Contact our chat support for online purchases support, product information, warranty support.

Fields marked with an asterisk are mandatory.

Your personal data will be processed according to HMD Global’s Privacy Policy and the HMD Support Supplement.

Email us

Tell us about your problem and we'll get back to you via email.

Contact us

Care centers

Prefer to bring your device in for our experts to have a look at? Find the location of your nearest Nokia & HMD phones, tablets and accessories care center.

Find a care center near you